Swali: Amesema (Ta´ala):

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

”Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.” (Yuunus 10 : 62)

Je, katika Aayah hii kuna dalili juu ya yale wanayoyasema kujuzu kujikurubisha kwa mawalii?

Jibu: Hapana. Ni kuwasifu tu kwa kuwa wameamini na wakamcha Allaah. Wakisifiwa ina maana kuwa wanaabudiwa badala ya Allaah? Mitume pia wamesifiwa ya kwamba wamemtii Allaah na wamefikisha ujumbe Wake. Elimu walionayo ni ya kwao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 39
  • Imechapishwa: 09/11/2016