Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote juu ya kwamba watu hawatomuona Mola wao katika maisha haya ya dunia. Kwa sababu nguvu zao haziwezi kumuona Allaah. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) Aakhirah atawaumba katika umbile la ukamilifu na uwezo ambao kwao wataweza kumuona Allaah (´Azza wa Jall). Yeye ndiye Muumbaji Mjuzi. Anafanya lile alitakalo (Subhaanahu wa Ta´ala).

Kutomuona duniani ni kwa sababu ya mtihani na majaribio. Kwa sababu mambo yaliyofichikana hakuna mwenye kuyaamini isipokuwa yule aliyewafikishwa na Allaah (´Azza wa Jall). Maaddiyyuun hawaamini isipokuwa yale wanayoyaona. Wanatofautiana na waumini juu ya kwamba wao wanaamini mambo yaliyofichikana. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewasifu katika Aayah juu ya kwamba wao wanaamini mambo yaliyofichikana. Miongoni mwa mambo hayo ni kuwa wao hawamuoni Allaah duniani katika maisha haya (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 53
  • Imechapishwa: 27/08/2020