Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya nne: Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Hapana! Hakika wao siku hiyo watawekewa kizuizi [wasimuone] Mola wao.” (83:15)

Dalili hapa ni kuwa amefanya (Subhaanahu wa Ta´ala) adhabu kubwa kwa makafiri ni kule kuzuiwa kumuona na kusikia Maneno Yake. ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) na maimamu wengine wametumia hoja kwa Aayah hii. at-Twabaraaniy na wengine wametaja kutoka kwa al-Muzaniy ambaye amesema: “Nimemsikia ash-Shaafi´iy akisema kuhusu Kauli Yake (´Azza wa Jall):

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Hapana! Hakika wao siku hiyo watawekewa kizuizi [wasimuone] Mola wao.” (83:15)

kuna dalili juu ya kwamba waumini na wenye kumcha Allaah watamuona Mola wao siku ya Qiyaamah.”

Kinachopata kufahamika hapa katika Aayah hii ni kinyume chake. Kinachotegemewa sio kinyume chake peke yake. Bali ni kitu kinachotiliwa nguvu na maandiko mengine mengi ambayo yamefikia kiwango cha Mutawaatir na dalili nyingine za Qur-aan tukufu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 54
  • Imechapishwa: 27/08/2020