Hawana kazi nyingine isipokuwa kuwaponda watawala

Miongoni mwa mambo ambayo watu wengi hawayatilii umuhimu ni kutowaheshimu watawala. Utakuja vikao vyao vingi wanawasema vibaya watawala. Lau maneno haya yangelikuwa na faida na yanatengeneza hali tungelisema ni sawa. Lakini hayana faida yoyote na hayatengenezi hali. Bali yanazichochea nafsi dhidi ya watawala, ni mamoja ikiwa ni wanazuoni au viongozi. Utakuta kuna watu hamu yao kubwa wanapokaa katika vikao ni kuvunja heshima za wanazuoni, waziri, mtawala au walio juu ya hao. Hili si sahihi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/427)