Tunachokataza ni kuwaponda watawala na si kuwanasihi

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho azungumze yaliyo na kheri au anayamaze.”[1]

La kushangaza ni kwamba baadhi ya watu lau utataka kumsema vibaya mtu wa kawaida miongoni mwa watu atakwambia usisengenyi ni haramu. Hawampi nafasi yeyote kuvunja heshima ya mwingine. Lakini ukivunja heshima ya mtawala miongoni mwa watawala wanaonelea kuwa kitendo hichi ni sawa. Mambo haya ni maradhi yalowapata watu wengi. Mimi ninazingatia kuwa ni maradhi. Ninamuomba Allaah atuponye nayo sisi na nyinyi kutokana na mambo haya ambayo watu wengi wamepewa mtihani kwayo. Kinyume chake lau watu wangelizuia ndimi zao na wakawanasihi watawala wao… Sisemi mtu anyamazie makosa. Mwandikie barua na umtumie mtawala. Hili ndio linalotakikana. Akifaidika na nasaha zako, hili ni jambo zuri. Na ikiwa hakufaidika na nasaha zako, madhambi yako kwake ikiwa kama ni kweli amefanya kosa. Na ikiwa barua hiyo haikumfikia, madhambi yako kwa yule aliyeizuia.

[1]al-Bukhaariy (6018) na Muslim (47).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/427-428)
  • Imechapishwa: 17/08/2025