Swali: Vipi kuhusu ambaye aliishi wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakini asikutane naye?

Jibu: Huyu haitwi ”Swahabah”, anaitwa ”Tabiy´”, kama vile as-Swunaabihiy na Ka’b al-Ahbaar, hawa wanaitwa ”Taabi´uun”, ingawa waliishi wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini hawakutana naye. Walikufa kabla ya kukutana naye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walifika Madiynah baada yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuaga kwake dunia.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25176/هل-يعد-صحابيا-من-ادرك-النبي-ولم-يلقه
  • Imechapishwa: 14/02/2025