Hatumfanyii Tabdiy´ yeyote ila anayetumbukia katika Bid´ah kwa kukusudia

Swali: Siku hizi tunasikia kanuni ikitajwa na wanafunzi nayo ni kuwa ikiwa humfanyii Tabdiy’ mtu binafsi wewe unachuja katika mfumo na wanawatahadharisha ndugu zao ambao hawafanyi hivyo.

Jibu: Sisi hatumfanyii Tabdiy’ ila mwenye kufanya Bid´ah kwa kukusudia. Akikusudia kufanya Bid´ah tunamfanyia Tabdi´ sawa akiwa ni mtu binafsi au kinyume chake. Lakini mwenye kufanya Bid´ah akidhani kuwa ndo haki kwa kutokujua , abainishiwe haki na Sunnah. Huu ndio mfumo wa Salaf.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.subulsalam.com/site/audios/alfozan/divers/130.Asalafiya7aqi qatoha-…
  • Imechapishwa: 09/04/2022