Hatua tatu anazotakiwa kufuata mwanafunzi wakati wa kulingania

Swali: Sisi ndio tunaanza likizo ya majira ya kipindi cha joto ambapo sisi na ndugu zetu wengine wanafunzi wanajiandaa kulingania katika dini ya Allaah sehemu mbalimbali nchini. Ni mamoja Quraanaa au kwenginepo. Ni zipi nasana zako kwa mwanafunzi wakati anapolingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall)? Ni hatua zipi anazotakiwa kufuata? Unamhimizi katika kitu gani?

Jibu: Kabla ya kila kitu awe na nia maalum. Wakati wa kuwalingania watu katika dini ya Allaah anatakiwa anuie kuieneza dini ya Allaah kati ya waja wa Allaah, amfunze mjinga na amwelekeza aliyepotea. Haya kabla ya kila kitu.

Pili: Anatakiwa alinganie kwa hekima, urafiki na upole na ajadili kwa njia nzuri pale ambapo kutahitajia mjadala.

Tatu: Asiingie ndani ya kitu asichokijua. Kwa mfano akajibu mambo asiyokuwa nayo elimu. Kutoa fatwa pasi na elimu ni miongoni mwa dhambi kubwa mno. Kwa sababu mtu anasema na anafutu juu ya Allaah. Kwa ajili hii Allaah (Ta´ala) ameambatanisha kitendo hicho na shirki pale aliposema (Ta´ala):

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Sema: “Hakika Mola wangu ameharamisha machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi [aina zote] na ukandamizaji bila ya haki. Na [ameharamisha] kumshirikisha Allaah kwa ambayo hakukiteremshia mamlaka na kuzungumza juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”[1]

Akiulizwa juu ya kitu asichokijua aseme “Sijui.” Lakini nawahakikishieni kwamba nitauliza na baadaye kuwafikishieni. Vilevile anaweza kumwelekeza kwa ambaye wanaweza kumuuliza ili dhimma yake iweze kutakasika. Lakini pamoja na hayo nasema kwamba: ikiwa anawalingania wengine na kufaidika kwake ni kukubwa kuliko anavyowafaidisha wengine katika kutoa mawaidha na kulingania katika dini ya Allaah, basi aendelee kujifunza elimu mpaka aive kisawasawa. Anaweza vilevile kukusanya kati ya mawili hayo.

[1] 07:33

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1465
  • Imechapishwa: 15/07/2020