السلام عليكم و رحمة الله و بركاته

Kuna mwanamke ambaye alikuwa hawezi kupata watoto na madaktari wakagundua kuwa ovari zake zimekufa. Madaktari wakampandikiza ovari baada ya hapo akapata ujauzito wa watoto wanne. Wakati mume alipopata taarifa hiyo akasema kuwa hataki watoto wanne kwa sababu kutamfanya mwanamke kuchoka na kudhoofika na akaomba watolewe watoto wawili na wabakizwe watoto wawili. Madaktari wakakataa kuavya mimba hiyo isipokuwa baada ya kupata fatwa kutoka kwa muheshimiwa Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. Mwanamke huyo yuko mwezi wa tatu sasa. Je, inafaa kwa madaktari kuavya mimba hiyo?

بسم الله الرحمن الرحيم

و عليكم السلام و رحمة الله و بركاته

Sintogusia suala la upandikizaji wa yai kwa sababu limeshapita

Kuhusu utoaji mimba, hapana neno ikiwa kunakhofiwa juu ya maisha ya mama na isitishe bado kipomoko hakijatimiza miezi minne. Ikiwa kipomoko kimeshatimiza miezi minne, basi haijuzu kuporomosha mimba kwa hali yoyote ile.

1420-07-16

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/29)
  • Imechapishwa: 10/07/2026