Mitikiso kwenye tupu ya nyuma inavunja wudhuu´?

Swali: Wakati wa swalah mtu anahisi harakati kwenye tupu ya nyuma bila ya kuhisi upepo au kusikia sauti. Je, inavunja wudhuu´?

Jibu: Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asitoke mmpaka asikie sauti au ahisi harufu.”[1]

Twahara ni yenye yakini na chenye kuvunja wudhuu´ kinatiliwa mashaka. Yakini haiondoki kwa shaka. Hii ni kanuni.

[1] al-Bukhaariy (137).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tahid-25-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017