Swali: Mwanaume amemuoa mwanamke ambapo akabaki kwa familia yake mwaka mzima kabla ya kufanya sherehe ya ndoa na kuhama pamoja. Je, analazimika kumhudumia katika kipindi hicho?
Jibu: Hapana. Asimuhudumie mpaka wahame pamoja. Muda wa kuwa hawajahama pamoja na sababu ni kutoka kwake yeye au familia yake, basi hakuna kinachomlazimu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
- Imechapishwa: 28/07/2023