Hapa ndipo unatakiwa kuiangalia nafsi yako mwenyewe

Swali: Ni vipi tutaoanisha Aayah inayosema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

“Enyi mlioamini! Ni juu yenu [majukumu ya] nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka, ikiwa mmeongoka. Kwa Allaah pekee ni marejeo yenu nyote, halafu atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.”[1]

na Hadiyth isemayo:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayaondoshe kwa mkono wake.”?

Jibu: Hakuna kati ya Aayah na Hadiyth mgongano. Wala hakuna kati ya Aayah na maneno Yake (Ta´ala):

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[2]

Aayah imefungamanishwa na uongofu wetu. Miongoni mwa kuongoka kwetu ni kuamrisha mema na kukataza maovu. Lakini ikiwa kuamrisha mema na kukataza maovu hakuwanufaishi kitu watu, basi mtu katika hali hiyo mtu aitengeneze nafsi yake mwenyewe. Ndio maana imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mtaamrishana mema na kukatazana maovu. Mtakapoona uchoyo wenye kutiiwa, matamanio yenye kufuatwa, dunia inapewa kipaumbele ambapo kila mmoja anapendezwa na maoni yake, basi ni juu yako kuiangalia nafsi yako na achana na jambo la watu wa kawaida.”[3]

Kwa hivyo Aayah isemayo:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

“Enyi mlioamini! Ni juu yenu [majukumu ya] nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka, ikiwa mmeongoka. Kwa Allaah pekee ni marejeo yenu nyote, halafu atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.”

inahusiana na pale mtu ambapo hawezi kuamrisha mema na kukataza maovu au kuamrisha mema na kukataza maovu hakusaidii kitu. Ndio maana Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) alisema:

“Enyi watu! Mnasoma Aayah hii na mnaifasiri kinyume na alivokusudia Allaah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ

“Enyi mlioamini! Ni juu yenu [majukumu ya] nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka, ikiwa mmeongoka.”

Hakika mimi nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakika watu watakapoona maovu na wasiyakataze, basi Allaah akaribia kuwaadhibu wote.”

[1] 5:105

[2] 03:104

[3] Abu Daawuud (4341), at-Tirmidhiy (3058) na Ibn Maajah (4014).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (31 A)
  • Imechapishwa: 20/05/2021