Wengi katika ndugu zetu Ahl-us-Sunnah hufikiria kwamba kila mwanachuoni anapoulizwa juu ya masuala fulani basi analazimika kumjibu muulizaji kwa kumfanyia muhadhara kutokana na Qur-aan na Sunnah. Dhana hii ni Bid´ah. Ni uzushi unaopingana na mfumo wa Salaf. Pindi Salaf walipokuwa wakiulizwa basi walikuwa wakinakili kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah. Lakini wakati swali linatokamana na ijtihaad na utambuzi wa vigezo na kanuni wanazozitambua tofauti na wengine, basi walikuwa wakitoa maoni yao vile wanavoona. Muulizaji anatakiwa kuchukua msimamo gani juu ya jawabu hilo? Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Hivyo basi waulizeni watu wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.”[1]

Kila muulizaji anao wajibu ambao ni kumuuliza mwanachuoni. Mwanachuoni kinachomlazimu ni kujibu. Jawabu linatofautiana. Wakati fulani linahitajia kutolewa dalili. Kwa msemo mwingine ikiwa dalili iko wazi na muulizaji anaelewa jawabu hilo. Wakati mwingine muulizaji ni mtu ambaye si msomi na hakuna anachoelewa isipokuwa jibu fupi kama vile “haramu”, “inajuzu”, “faradhi”, “swalah ni batili”, “swalah imesihi” na mfano wa hivo. Hapa ndipo ambapo tunapasa kupambanua kwa sababu tunalazimika kuwazungumzisha watu kwa kiasi cha akili yao.

Hapa ndipo kunabainika jumla ambayo mara nyingi naisema juu ya Da´wah yetu: Qur-aan, Sunnah na Salaf. Kwa sababu kupitia mfumo wao ndio tutaelewa majibu haya yaliyomakinika na kupambanuliwa.

[1] 16:43

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naasir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (875)
  • Imechapishwa: 21/05/2021