Hapa ndipo mtu asimame wakati wa Iqaamah

Swali: Ni lini imewekwa katika Shari´ah kuinuka wakati kunapokimiwa swalah? Je, ni wakati wa maneno maalum?

Jibu: Wanasema kuwa imependekezwa kusimama pale muadhini anaposema:

قد قامت الصلاة

“Swalah imesimama.”

Lakini hata hivyo sijui dalili yoyote juu ya hili. Asimame pale itapomkuia sahali kwake kusimama. Baadhi ya wengine wanasema asimame pale atapomuona imamu anasimama.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 06/01/2017