Swali: Je, ni katika haki ya wanachuoni kumwambia mtu maalum ya kwamba ni kafiri na kumtuhumu ukafiri?

Jibu: Kumkufurisha kwa jumla ni kitu kilichowekwa katika Shari´ah. Kwa mfano mtu akasema kuwa yule mwenye kutaka uokozi kwa asiyekuwa Allaah katika mambo ambayo ni haki ya Allaah Pekee, ni kafiri. Mfano wa hilo ni kama mwenye kutaka uokozi kutoka kwa Mtume miongoni mwa Mitume wa Allaah au walii amponye au amponye mtoto wake.

Hali kadhalika kumkufurisha mtu kwa dhati yake akipinga kitu ambacho kinajulikana fika uwepo wake katika Uislamu. Baadhi ya mambo hayo ni kama swalah, zakaah au swawm. Baada ya kufahamishwa ni wajibu [kumkufurisha akiendelea kupinga]. Anatakiwa kunasihiwa, akitubu ni sawa, la sivyo ni wajibu kwa mtawala kumuua hali ya kuwa ni kafiri.

Lau kumkufurisha mtu kwa dhati yake pale kunapopatikana kitu kinachowajibisha kufuru ingelikuwa ni kitu ambacho hakikuwekwa katika Shari´ah basi kusingesimamishwa adhabu ya Kishari´ah kwa wenye kuritadi kutoka katika Uislamu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/93-94)
  • Imechapishwa: 24/08/2020