Hapa ndipo itafaa kwa mwanamke kujiozesha mwenyewe

Swali: Vipi ikiwa mwolewaji hana walii wala mtawala kabisa?

Jibu: Atajiozesha mwenyewe. Ni vyema zaidi ikiwezekana kuozeshwa na raisi  wa kituo cha Kiislamu au mtu mfano wake, kwa sababu mtu huyu anasimama nafasi ya mtawala. Hali kama hiyo inaweza kutokea USA na mfano wake. Raisi wa kituo cha Kiislamu anamfaa akipata mwanaume anayelingana naye.  Isipowezekana atajiozesha mwenyewe kutokana na dharurah na kwa uhudhuriaji wa mashahidi wawili. Atamweleza kuwa amejiozesha kwake mwenyewe na kwamba amekubali pamoja na kuhudhuria mashahidi wawili na kuwepo mahari.

Swali: Akipatikana muislamu – ingawa sio mtawala – inafaa kwa mwanamke kumuwakilisha?

Jibu: Haimlazimu mwanamke huyo, kwa sababu sio walii wake. Lakini hapana vibaya endapo atamuwakilisha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23839/حكم-زواج-من-ليس-لها-ولي-ولا-حاكم
  • Imechapishwa: 18/05/2024