Swali: Vipi kuhusu kurefusha nywele za kichwani?

Jibu: Msigni wake ni kwamba inajuzu. Waarabu walikuwa wakirefusha nywele zao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiacha nywele zake na wakati mwingine zilifika mabegani na wakati mwingine zilikuwa fupi kulingana na alivyozinyoa alipokuwa katika Hijjah au ´Umrah. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akizinyoa katika Hijjah na kuzipunguza katika ´Umrah. Kwa hiyo mtu akizirefusha bila kusudio baya, si kwa ajili ya wanawake wala kwa ajili ya fitina, basi hakuna dhambi katika hilo. Lakini kama kuzi­refusha katika mji au kijiji fulani kunamfanya atuhumiwe kwa ubaya au watu wamdhanie vibaya, basi inafaa aache kufanya hivo ili asituhumiwe kwa uovu. Kama anazirefusha kwa ajili ya wanawake, fitina na kuwachezea wanawake, basi hilo ni jambo la maovu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2445/حكم-اطالة-شعر-الراس
  • Imechapishwa: 29/03/2026