Hapa ndipo itafaa kumkosoa Khatwiyb mbele za watu

Swali: Khatwiyb akikosea katika Khutbah yake akosolewe na kuambiwa kuwa amekosea mbele ya watu?

Jibu: Ikiwa kosa lake ni la wazi na linaenda kinyume na Shari´ah. Lakini iwe kwa maneno mazuri. Lakini ikiwa ni kosa jepesi haidhuru. Kama vile kosa la kisarufi na mfano wake, ni kitu chepesi. Ama ikiwa amehalalisha haramu au amewajibisha ambacho sio wajibu, ni sawa akabainishiwa kwa mujibu wa dalili za Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23845/هل-يرد-على-الخطيب-اذا-اخطا-في-الخطبة
  • Imechapishwa: 17/05/2024