Hapa ndipo inachukiza kuswali kati ya nguzo


Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya ambaye ameswali kati ya nguzo pasi na dharurah hali ya kutojua au kwa kujua?

Jibu: Inachukiza kuswali kati nguzo zinapokatika safu kukiwa hakuna haja. Ikiwa kuna haja, kama ufinyo wa msikiti, basi yanaondoka machukizo. Vivyo hivyo yanaondoka machukizo ikiwa hakupelekei kukatika kwa safu.

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (06/330) nr. (20977)
  • Imechapishwa: 13/05/2022