Hapa ndipo anayekodisha ataanza kuhesabu zakaah ya kodi ya nyumba

Swali: Kuna mtu yuko na nyumba au duka analokodisha. Je, ataanza kuhesabu ulipaji wa zakaah kuanzia pale walipoandika mkataba au kuanzia pale atapoanza kupokea kodi?

Jibu: Ataanza kuhesabu kuanzia pale kumeandikwa mkataba. Kwa sababu kodi inathibiti kwa mkataba. Kukishapatikana manufaa, kodi ikaingia na mkataba ukatimiza mwaka mzima, basi hapo atawajibika kutoa zakaah yake. Lakini endapo mwenye nyumba atapa kodi katikati ya mwaka na akatumia pesa hizo kabla ya kukamilika mwaka, basi halazimiki kuitolea kodi hiyo zakaah. Kwa mfano anakodisha duka hilo kwa pesa 10.000 na akapata pesa 5.000 baada ya kupita nusu mwaka kisha akazitumia, hatozitolea zakaah zile pesa 5.000 kwa sababu hazikukamilisha mwaka tangu kuandikwa kwa mkataba. Hata hivyo atalazimika kuzitolea zakaah zile pesa 5.000 zingine ambazo amepata baada ya kupita mwaka.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/19-20)
  • Imechapishwa: 17/05/2026