Huenda mtawala amechukua utawala kupitia mapinduzi ya kijeshi katika maeneo fulani ambapo watu wakashindwa kumzuia. Hata kama amempindua kiongozi wa Kiislamu kisha baadaye akadhibiti utawala juu ya eneo hilo, haitakiwi kukabiliana naye baada ya hapo. Iwapo waislamu waliokuwa wakiishi chini ya yule khaliyfah wa kwanza wataweza kujitetea dhidi ya mashambulizi, watafanya hivo ijapo ni kwa kumuua yule mshambuliaji. Lakini wasipoweza kukabiliana naye na yule mvamizi akashika madaraka, basi haitojuzu kwao kusababisha machafuko katika jamii. Hilo ni kutokana na sababu mbili:
1 – Wanaenda kinyume na Sunnah inayoamrisha kumsikiliza na kumtii katika yote yaliyo mema ijapo ni mtawala huyo mpya ameshinda kwa mapinduzi ya kijeshi.
2 – Wanaziweka nafsi zao katika khatari ya kumwagwa damu zao, kuvunjwa heshima zao, kuporwa mali zao na kuleta fitina katika yale maeneo wanayoeshi.
Kwa ajili hiyo ni lazima kujisalimisha, kumpa kiapo cha utiifu na kuswali nyuma yake na nyuma ya manaibu wake na wale aliowateua kama mahakimu, maafisa wa polisi, maimamu wa misikiti na viongozi wa makabila. Ni lazima kwa raia kujisalimisha kwa watu hawa na kwa watu mfano wao. Huu ndio mfumo wa Ahl-uis-Sunnah wal-Jamaa´ah tofauti na mfumo wa Khawaarij. Khawaarij wanaenda kinyume na Ahl-us-Sunnah katika jambo hili na mambo mengine yote kwa sababu ya ujinga wao khatari, kukimbia duara za kielimu na kupuuza nasaha za wanazuoni. Hivi ndivo wanavokuwa Khawaarij wote katika kila zama na kila pahali. Wanakuwa na msiimamo mikali na wanakuwa hawana elimu, hekima na ufahamu.
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 128
Huenda mtawala amechukua utawala kupitia mapinduzi ya kijeshi katika maeneo fulani ambapo watu wakashindwa kumzuia. Hata kama amempindua kiongozi wa Kiislamu kisha baadaye akadhibiti utawala juu ya eneo hilo, haitakiwi kukabiliana naye baada ya hapo. Iwapo waislamu waliokuwa wakiishi chini ya yule khaliyfah wa kwanza wataweza kujitetea dhidi ya mashambulizi, watafanya hivo ijapo ni kwa kumuua yule mshambuliaji. Lakini wasipoweza kukabiliana naye na yule mvamizi akashika madaraka, basi haitojuzu kwao kusababisha machafuko katika jamii. Hilo ni kutokana na sababu mbili:
1 – Wanaenda kinyume na Sunnah inayoamrisha kumsikiliza na kumtii katika yote yaliyo mema ijapo ni mtawala huyo mpya ameshinda kwa mapinduzi ya kijeshi.
2 – Wanaziweka nafsi zao katika khatari ya kumwagwa damu zao, kuvunjwa heshima zao, kuporwa mali zao na kuleta fitina katika yale maeneo wanayoeshi.
Kwa ajili hiyo ni lazima kujisalimisha, kumpa kiapo cha utiifu na kuswali nyuma yake na nyuma ya manaibu wake na wale aliowateua kama mahakimu, maafisa wa polisi, maimamu wa misikiti na viongozi wa makabila. Ni lazima kwa raia kujisalimisha kwa watu hawa na kwa watu mfano wao. Huu ndio mfumo wa Ahl-uis-Sunnah wal-Jamaa´ah tofauti na mfumo wa Khawaarij. Khawaarij wanaenda kinyume na Ahl-us-Sunnah katika jambo hili na mambo mengine yote kwa sababu ya ujinga wao khatari, kukimbia duara za kielimu na kupuuza nasaha za wanazuoni. Hivi ndivo wanavokuwa Khawaarij wote katika kila zama na kila pahali. Wanakuwa na msiimamo mikali na wanakuwa hawana elimu, hekima na ufahamu.
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 128
https://firqatunnajia.com/50-utawala-uliofikiwa-kwa-mapinduzi-ya-kijeshi/