Khaliyfah au mtawala ni yule aliyechaguliwa na watu wenye busara na wenye elimu ili awe kiongozi wa waislamu. Haijalishi kitu mtu huyo ni kiongozi wa waislamu wote, kama walivyokuwa makhaliyfah waongofu, au maeneo fulani, kama ilivyo hivi sasa na hapo kitambo. Muda wa kuwa ni muislamu, basi anazingatiwa kuwa ndiye mtawala na kiongozi wa maeneo hayo ambayo amepewa kiapo cha utiifu. Kwa msemo mwingine ni lazima kwa watu wa maeneo hayo kumtii katika yaliyo mema, kutimiza kiapo chake, kushirikiana naye katika matendo mema na kuondosha ili kuwasiadia wananchi kuishi kwa amani na utulivu. Hilo limekuwa daima ni lengo muhimu katika historia ya wanadamu.

Haijuzu kwa yeyote kumfanyia uasi. Yule mwenye kufanya uasi dhidi yake ambapo akafa, basi amekufa kifo cha kipindi kabla ya kuja Uislamu. Katika kipindi kabla ya kuja Uislamu mtu hakuwa akiwanyenyekea wala kuwatii viongozi wao. Hatuma maana kwamba ni kafiri – bado ni muislamu – muda wa kuwa Bid´ah zake sio za kukufurisha. Hata hivyo ni mzushi aliyepinda kutokana na haki, na akifa hali ya kuwa ni mwenye kumfanyia uasi kiongozi wake, amekufa kifo cha kipindi kabla ya kuja Uislamu. Kwa msemo mwingine kama vile vifo walivyokufa wale watu waliokufa kabla ya kuja Uislamu pasi na kuwa na mamlaka yoyote juu yao, au kwamba walikuwa na mamlaka lakini hata hivyo wakiishi katika maisha ya vurugu, umwagaji damu na uporaji. Muislamu hachukui msimamo huo juu ya kiongozi wake muislamu, anayehukumu kwa Shari´ah, kuwaletea amani wao na njia zao na kutekeleza alama za Kiislamu katika jamii na hivyo wankuwa na kheri duniani na Aakhirah. Bila ya mtawala watu hawawezi kufikia kheri yoyote, kwa sababu watu wanaishi wakiwa na khofu juu ya nafsi zao, familia zao na mali zao. Haya anayajua yule mwenye kusoma historia.

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 127-128
  • Imechapishwa: 17/05/2026