Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Yule anayefanya uasi dhidi ya kiongozi wa waislamu ambaye watu wamekusanyika juu yake na wakakubali ukhaliyfah wake kwa njia yoyote ile, kwa kuridhia au kwa nguvu, amewatawanyisha waislamu na ameenda kinyume na mapokezi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfanya uasi huyu akifa katika hali hii, basi amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri.
MAELEZO
Huu ni msingi muhimu unaothibitisha mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Nao ni kwamba ni lazima kumsikiliza na kumtii mtawala wa Kiislamu katika yaliyo mema. Vilevile ni haramu kumfanyia uasi kwa aina yoyote ile – si kwa maneno yanayowachochea raia dhidi yake wala kwa silaha. Yote haya ni katika matendo ya Khawaarij kama ninavosema mara nyingi. Maimamu wamesema kuwa mambo kama haya ya uasi dhidi ya watawala wa Kiislamu wanyanyasaji na madhalimu kwamba ni katika matendo ya Khawaarij. Ahl-us-Sunnah hawana mfumo huo. Ahl-us-Sunnah wana mfumo uliosalimika na wenye hekima pale wanapowaombea du´aa viongozi, kumnasihi kwa njia sahihi na kushirikiana naye katika kuthibitisha zile nembo za Kiislamu na Sunnah katika jamii na kueneza elimu katika misikiti na maeneo mengine. Huu ndio mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah tofauti na Khawaarij waliochupa mipaka na waasi ambao wanawafanyia uasi watawala wao kwa sababu ya dhuluma na ukandamizi wao. Aidha haifai ni mamoja dhuluma hiyo imethibiti kikweli au ni madai tu kutoka kwa makhaini, watu wanaopenda kueneza maharibifu ulimwenguni na kuchochea fitina katika jamii za Kiislamu. Kwa hivyo ambaye anafanya uasi dhidi ya kiongozi au khaliyfah baada ya kumakinika utawala wake maeneo fulani, ni miongoni mwa Khawaarij ambao kila mmoja analazimika kumkataa na kwenda kinyume naye. Ahl-us-Sunnah wanapaswa kuhimiza kupambana nao bega kwa bega pamoja na mtawala wa Kiislamu. Pepo kwa yule mwenye kuwaua au wakauliwa nao, kama ilivyosihi kutoka kwa kiongozi wa watu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 126-126
- Imechapishwa: 17/05/2026

Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 126-126
Imechapishwa: 17/05/2026
https://firqatunnajia.com/48-tofauti-na-ahl-us-sunnah-na-khawaarij/