Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Swalah ya ijumaa nyuma yao na nyuma ya magavana wao inafaa na ni timilifu na ni Rak´ah mbili. Yule mwenye kuirudi ni mtu wa Bid´ah mwenye kuyaacha mapokezi na anaenda kinyume na Sunnah. Hapati chochote katika fadhila za ijumaa midhali haonelei kuwa ni sahihi kuswali swalah ya ijumaa nyuma ya viongozi sawa wawe wema au waovu. Sunnah ni kuswali Rak´ah mbili pamoja nao na kuonelea kuwa ni timilifu. Usiwe na shaka kwenye kifua chako juu ya hilo.
MAELEZO
Huu ni msingi mwingine wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah unaobainisha ´Aqiydah na mfumo wao kuhusiana na viongozi wa waislamu, ni mamoja ni wema au waovu. Wanaona kufaa, bali ni lazima kuswali swalah ya ijumaa na swalah za ´iyd mbili. Haijuzu mtu akaacha kufanya hivo kwa hoja eti ni dhalimu au mkandamizi. Yule mwenye kuacha swalah ya ijumaa au swalah za mkusanyiko zinazoswalishwa na viongozi au manaibu wao ni mzushi, na ambaye ataswali nyuma yao ndiye anafuata Sunnah.
Aidha haijuzu kuirudia baadaye kama wanavofanya Ahl-ul-Bid´ah. Swalah ya ijumaa itaswaliwa Rak´ah mbili kama ilivyofaradhishwa. Wala haijuzu baadaye kuiswali tena Dhuhr hata kama kiongozi au manaibu wao ni madhalimu na wanyanyasaji.
Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, kundi lililookoka na kunusuriwa. Tofauti na Khawaarij ambao hawaoni kufaa kuswali nyuma ya viongozi ambao ni madhalimu na wakandamizi; bali wanamkufurisha. Vivyo hivyo Raafidhwah wanaswali Dhuhr punde tu baada ya kumaliza kuswali swalah ya ijumaa. Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye amewapambanua Ahl-us-Sunnah kwa Shari´ah ilio kati na kati baina ya uchupaji mpaka na uzembeaji.
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 124-125
- Imechapishwa: 17/05/2026
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Swalah ya ijumaa nyuma yao na nyuma ya magavana wao inafaa na ni timilifu na ni Rak´ah mbili. Yule mwenye kuirudi ni mtu wa Bid´ah mwenye kuyaacha mapokezi na anaenda kinyume na Sunnah. Hapati chochote katika fadhila za ijumaa midhali haonelei kuwa ni sahihi kuswali swalah ya ijumaa nyuma ya viongozi sawa wawe wema au waovu. Sunnah ni kuswali Rak´ah mbili pamoja nao na kuonelea kuwa ni timilifu. Usiwe na shaka kwenye kifua chako juu ya hilo.
MAELEZO
Huu ni msingi mwingine wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah unaobainisha ´Aqiydah na mfumo wao kuhusiana na viongozi wa waislamu, ni mamoja ni wema au waovu. Wanaona kufaa, bali ni lazima kuswali swalah ya ijumaa na swalah za ´iyd mbili. Haijuzu mtu akaacha kufanya hivo kwa hoja eti ni dhalimu au mkandamizi. Yule mwenye kuacha swalah ya ijumaa au swalah za mkusanyiko zinazoswalishwa na viongozi au manaibu wao ni mzushi, na ambaye ataswali nyuma yao ndiye anafuata Sunnah.
Aidha haijuzu kuirudia baadaye kama wanavofanya Ahl-ul-Bid´ah. Swalah ya ijumaa itaswaliwa Rak´ah mbili kama ilivyofaradhishwa. Wala haijuzu baadaye kuiswali tena Dhuhr hata kama kiongozi au manaibu wao ni madhalimu na wanyanyasaji.
Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, kundi lililookoka na kunusuriwa. Tofauti na Khawaarij ambao hawaoni kufaa kuswali nyuma ya viongozi ambao ni madhalimu na wakandamizi; bali wanamkufurisha. Vivyo hivyo Raafidhwah wanaswali Dhuhr punde tu baada ya kumaliza kuswali swalah ya ijumaa. Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye amewapambanua Ahl-us-Sunnah kwa Shari´ah ilio kati na kati baina ya uchupaji mpaka na uzembeaji.
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 124-125
Imechapishwa: 17/05/2026
https://firqatunnajia.com/47-swalah-nyuma-ya-viongozi/