Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye haswali kabisa?
Jibu: Ambaye haswali ni ameritadi katika Uislamu na ni mwenye kumkufuru Allaah ukafiri wenye kumtoa katika dini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Baina ya mtu na kufuru na shirki ni kuacha swalah.”[1]
Kuacha swalah kunapelekea katika matokeo kadhaa ya kilimwengu na ya Aakhirah. Kuhusu matokeo ya kilimwengu:
1 – Ni wajibu kwa mamlaka kumlingania mtu huyo katika Uislamu. Akitubia hali ya kumtakasia nia Allaah (Ta´ala) na akaanza kuswali, basi Allaah atamkubalia swalah yake, vinginevyo atauliwa hali ya kuwa ni kafiri na mwenye kuritadi.
2 – Haifai kwa yeyote kumuozesha. Akiozeshwa, basi ndoa hiyo ni batili na mke hawi halali kwake.
3 – Mke wake ambaye anaishi naye anakuwa ni haramu kwake. Ndoa yao inafutwa na hivyo ni wajibu kuwatenganisha mpaka arudi katika Uislamu.
4 – Kichinjwa chake si halali na nyama yake haitakiwi kuliwa. Sambamba na hilo kichinjwa cha myahudi na mkristo kinaliwa.
5 – Akifa mtu katika jamaa zake, haifai kumrithi. Akifa, hakuna yeyote katika jamaa zake ambaye atamrithi. Badala yake mali yake itapelekwa katika mfuko wa serikali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Muislamu hamrithi kafiri na wala kafiri hamrithi muislamu.”[2]
6 – Si halali kwake kuingia mipaka ya Makkah.
7 – Hakuna chochote kinachokubaliwa katika matendo yake mema, si swadaqah, swawm, hijjah wala kitu kingine.
8 – Akifa hatooshwa na wala hatovikwa sanda. Hatozikwa kwenye makaburi ya waislamu na wala hatoombewa du´aa ya rehema na msamaha. Haifai kwa ndugu yake yoyote anayejua hali yake kupeleka jeneza lake kwa waislamu ili wamswalie au kumzika kwenye makaburi yao. Hakika mambo yalivyo ni kwamba atafutiwe shimo na kuzikwa mahali hapo.
Kuhusu matokeo ya Aakhirah ni kama yafuatayo:
1 – Ataadhibiwa ndani ya kaburi adhabu kali kama watavyoadhibiwa makafiri wengine wote au zaidi ya hivyo.
2 – Siku ya Qiyaamah atafufuliwa na Fir´awn, Haamaan, Qaaruun na Ubayy bin Khalaf.
3 – Atadumishwa ndani ya Moto milele.
[1] Muslim (82).
[2] al-Bukhaariy (6764) na Muslim (1614).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/99-101)
- Imechapishwa: 17/05/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/99-101)
Imechapishwa: 17/05/2026
https://firqatunnajia.com/asiyeswali-kabisa/