Swali: Kuna Swahabah aliyechimba kaburi la baba yake. Je, inajulisha kufaa kwa jambo hilo?

Jibu: Huyu ni Jaabir bin ´Abdillaah. Ikiwa mtu anaona kuwa kuna maslahi; kwa mfano maeneo si pazuri, mafuriko, njia au sehemu moja wamezikwa wawili na akataka kumtenganisha kila mmoja kivyake, hapana neno kutokana na maslahi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumkemea Jaabir.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23179/هل-يجوز-نبش-القبر
  • Imechapishwa: 23/11/2023