Hakuna udhuru katika kutokujua mambo ya Kiislamu ya wazi

Swali: Je, ni lazima kumsimamishia hoja mwenye kufanya kitu kinachovunja Uislamu kabla ya kufanyiwa Takfiyr? Je, inajuzu kumtakia rehema akifa kabla ya kusimamikiwa na hoja?

Jibu: Ikiwa kuritadi kunahusiana na mambo ya wazi, kama kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall), kumtukana Allaah na Mtume Wake na mfano wa hayo, haya ni mambo ya wazi na hakuna ujinga ndani yake. Mambo kama haya ataambiwa atubie. Kama hakutubia anahukumiwa kuwa ameritadi na hivyo anauawa.

Kuhusiana na mambo yaliyojificha ambayo yanahitajia kubainishwa, haya ni lazima abainishiwe. Hahukumiwi kuritadi mpaka abainishiwe kwa kuwa ni mambo yaliyojificha kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-14.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020