Mababu zetu kama Ahmad bin Hanbal hawakutoka na kufanya mapinduzi na migomo. Wakati Ahl-ul-Hadiyth walipokusanyika kwake katika mnasaba wa fitina ya kuumbwa kwa Qur-aan na kumuuliza kama inajuzu kufanya uasi aliwaamrisha kutotoka kwake, kumcha Allaah na kutosema hivo.
Wanafunzi! Tulieni na waulizeni wanachuoni wenu kama Shaykh Ibn Baaz na Shaykh al-Albaaniy. Anayewatukana wanachuoni kama tulivyosema ima ni Hizbiy, mpumbavu mmoja mdogo au mtu wa Bid´ah.
Ninawapa changamoto ya kuja na Sunniy mmoja anayemdharau Shaykh ´Abdul-´Aziyz. Je, Shaykh Rabiy´ bin Haadiy anamdharau Shaykh Ibn Baaz? Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad anamdharau Shaykh Ibn Baaz? Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthyamiyn anamdharau Shaykh Ibn Baaz?
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 31-32
- Imechapishwa: 26/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)