Swali: Profesa mmoja ametwambia kwamba kuhajiri hakuna hii leo kwa sababu hakuna nchi ya Kiislamu mahali kokote ulimwenguni. Je, maneno yake ni sahihi?

Jibu: Hivo ndivo wanavosema Takfiyriyyuun ambao wanawakufurisha watu wote. Huyu anasema kuwa hakuna nchi ya Kiislamu ulimwenguni kote; huku ni kukufurisha kwa jumla. Haya ni maneno batili. Isitoshe muislamu anatakiwa kuhajiri na waislamu wenzake hata kama hawana nchi; anatakiwa kuwa pamoja na waislamu wenzake na asiwe pamoja na makafiri, ni mamoja wanaenda katika nchi ya Kiislamu au waislamu walioko hapo ndio wachache walioshikamana na dini yao. Ima mtu anahajiri katika nchi ya Kiislamu ambayo inahukumu kwa Shari´ah, jambo ambalo ndio msingi na linalotakikana, au anahajiri kwenda kwa waislamu na kukaa na kuishi nao, kuwalea watoto wake pamoja na watoto wao na kuwa katika mazingira ya Kiislamu. Anaweza vilevile kuhajiri kwenda katika nchi ya kikafiri ambayo ina madhara madogo kuliko nchi yenye kudhulumu na kandamizi. Hivo ndivo walivofanya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati walipohajiri kwenda Uhabeshi ambao mfalme wake alikuwa ni an-Najaashiy ambaye alikuwa mnaswara na baada ya hapo akasilimu. Mtu anatakiwa kutafuta kuhajiri, ima kuhajiri kikamilifu katika nchi ya Kiislamu ambayo inahukumu kwa Shari´ah, jambo ambalo ndio msingi na ndio linalotakikana, au angalau kwa uchache afanye lile ambalo lina madhara madogo na ahamie kwa waislamu au katika nchi yenye madhara madogo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=n8YaDaZLOG4
  • Imechapishwa: 29/03/2024