Nilimuuza Ahmad kuhusu mwanamke ambaye ni muasi kwa mume wake ana haki ya matumizi. Akajibu:

Hapana.

Haaruun kasema:

Nilimuuza al-Hasan [al-Baswriy] kuhusu mwanamke ambaye ametoka nje ya nyumba licha ya kwamba mume amemkataza hilo na kama ana haki ya kuhudumiwa. Akasema: Ndiyo. Nikamuuliza ni kitu gani atamuhudumia kwacho. Akajibu: Mauwa ya mchanga.

Twariq kasema:

ash-Sha’biy aliulizwa kuhusu mwanamke ambaye ni muasi kwa mume wake. Akajibu: Hana haki yoyote ya matumizi hata kama ataeshi pamoja naye kwa miaka ishirini.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaail-ul-Imaam Ahmad bin Hanbal, uk. 247
  • Imechapishwa: 22/09/2020