Haki haikubaliwi kwa kuangalia wingi wa wafuasi

Swali: Je, kutumiwe dalili ya wingi wa watu katika kuikubali haki?

Jibu: Wingi wa watu sio dalili. Dalili zinatambulika kwa maana ya kile kilichowekwa na dalili za Shari´ah na si kwa wingi:

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ

“Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi.” (12:103)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23458/هل-يستشهد-بالكثرة-على-قبول-الحق
  • Imechapishwa: 25/01/2024