Haikuthibiti kutoka kwa Mtume wala Maswahabah

Swali: Kuapa kwa msahafu kunahesabiwa ni shirki?

Jibu: Akikusudia yale maneno yaliyomo ndani yake haizingatiwi ni shirki. Na akikusudia yale makaratasi, ngozi na wino inazingatiwa ni shirki. Kwani vitu hivyo vimeumbwa. Hata hivyo ni shirki ndogo:

“Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah amekufuru au amefanya shirki.”

Kwa hali yoyote kuapa kwa Qur-aan ni jambo halikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 24
  • Imechapishwa: 18/01/2025