Swali: Kuna muislamu amemwambia ndugu yake kuwa ni kafiri pamoja na kuwa aliyeambiwa hivyo anaswali vipindi vitano na kuswali. Ni ipi hukumu na ni ipi dawa ya kusahau sana?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu kumpachika ndugu yake kufuru ikiwa hakufanya kitu hicho. Ni wajibu kwake kutubu na kumuomba msamaha Allaah pamoja na kumtaka radhi ndugu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametishia hilo katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh.

Kuhusu namna ya kutibu kusahau na kuhifadhi ni kumcha Allaah (´Azza wa Jall), kudumu kwa kurejelea na kukariri vile unavyotaka kuvihifadhi. Pamoja na kumuomba Allaah akusaidie juu ya hilo. Tunamuomba Allaah akupe wewe na sisi mafanikio katika kuhakikisha yale uliyoyakusudia.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/91)
  • Imechapishwa: 24/08/2020