Haijuzu kwa mtu kuchelewesha hajj ilihali ana uwezo

Swali: Mimi nina miaka thelathini. Je, inajuzu kwangu kuchelewesha hajj mpaka mwaka ujao ilihali ninaweza kuhiji hivi sasa?

Jibu: Hapana, haijuzu. Yule ambaye ana uwezo wa kufanya hajj basi ni anawajibika kuikimbilia. Kwa sababu mtu hajui anaweza kufikwa na nini. Huenda akapoteza pesa hii. Huenda akawa mgonjwa katika mustakabali. Huenda akafa. Kwa hivyo yule ambaye ana uwezo wa kufanya hajj basi ni anawajibika kuikimbilia. Haijuzu kwake akaichelewesha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/944
  • Imechapishwa: 09/12/2018