Haichukizi, bali inapendeza

Swali: Baadhi wanaifasiri Hadiyth hii ya kwamba Siwaak inachukiza mwishoni mwa mchana?

Jibu: Ni nyonge. Baadhi ya watu wanaona kuwa inachukiza. Lakini maoni ya sawa ni kwamba haichukizi, kwa sababu hakuondoshi ile harufu. Ile harufu ya mfungaji inatokea tumboni. Kutumia Siwaak kunapendeza kwa muumini katika nyakati zote hata kama amefunga. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitumia Siwaak nyakati zote. Anasema:

Siwaak inasafisha mdomo na inamridhisha Mola.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Lau kama sio kuwatia uzito ummah wangu, basi ningeliwafaradhishia kutumia Siwaak wakati wa kila swalah kama walivyofaradhishiwa kutawadha.”[2]

Hapa kunaingia pia swalah ya ´Aswr na Dhuhr kwa mfungaji. Kwa hivyo sahihi ni kwamba haichukizi kwa mfungaji kutumia Siwaak katika nyakati zote. Bali inapendeza.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (209)

[2] Swahiyh kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (208)

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24109/ما-حكم-السواك-للصاىم
  • Imechapishwa: 31/08/2024