Ibn Baaz kuhusu anayeanza kuosha upande wa kushoto kabla ya wa kulia

Swali: Vipi ikiwa mwenye kutawadha ataanza kuosha mkono wa kushoto kabla ya mkono wa kulia?

Jibu: Sahihi ni kwamba haijuzu. Kuna makinzano yanayotambulika. Wengi wanaona kuwa ni kwa njia ya mapendekezo. Hata hivyo kule Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kudumu kutanguliza mkono na mguu wa kulia kabla ya wa kushoto – na yeye ndiye mwenye kufasiri yale yanayotajwa njia ya kuenea ndani ya Qur-aan – kunafahamisha kuwa na nguvu yale maoni ya waliosema kuwa ni wajibu kuanza na upande wa kulia. Imekuja katika Hadiyth ya Abu Hurayrah:

“Mkivaa na kutawadha basi anzeni na upande wenu wa kulia.”

 Kwa kufupisha ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefasiri Aayah inayosema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ

“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na panguseni kwa [kupaka maji] vichwa vyenu na [osheni] miguu yenu hadi vifundoni.” (05:06)

Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye anafasiri; ameanza na upande wa kulia katika kuosha mikono yake na miguu yake. Kwa hiyo ni wajibu kuanza na hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24108/حكم-تقديم-اليسرى-على-اليمنى-في-الوضوء
  • Imechapishwa: 31/08/2024