Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
164 –
عَنْهُ أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم أَمَرَ بِلَعْقِ الأَصَابِعِ وَالصَّحْفَةِ، وَقَالَ: (إنَّكُمْ لا تَدْرونَ في أَيِّها البَرَكَةُ). رواه مسلم
Jaabir bin ´Abdilaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuramba vidole na sahani na kusema “Hakika nyinyi hamjui baraka iko wapi”.”[1]
Katika upokezi mwingine imekuja:
إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أَحَدِكُمْ فَلْيَأخُذْهَا، فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذىً، وَلْيَأكُلْهَا وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيطَانِ، وَلا يَمْسَحْ يَدَهُ بالمنْدِيلِ حَتَّى يَلْعَقَ أصَابعَهُ فَإِنَّهُ لا يَدْرِي في أيِّ طَعَامِهِ البَرَكَةُ
“Mmoja wenu anapoponyokwa na chakula aokote na aondoshe palipopatwa na uchafu na halafu alile na asimwachie nalo shaytwaan. Asipanguse mkono wake na taulo mpaka arambe kwanza vidole vyake. Kwani hakika hajui ni wapi baraka ilipo.”[2]
Katika upokezi mwingine imekuja:
إنَّ الشَّيطَانَ يَحْضُرُ أَحَدَكُمْ عِنْدَ كُلِّ شَيءٍ مِنْ شَأنِهِ، حَتَّى يَحْضُرَهُ عِنْدَ طَعَامِهِ، فَإذَ سَقَطَتْ مِنْ أَحَدِكُمْ اللُّقْمَةُ فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذَىً، فَلْيَأكُلْهَا وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيطَانِ
“Hakika shaytwaan humwendea mmoja wenu katika kila jambo miongoni mwa mambo yake mpaka wakati wa kula. Mmoja wenu anapoponyokwa na chakula aondoshe palipopatwa na uchafu kisha alile na asimwachie nalo shaytwaan.”[3]
Hapa kuna adabu mbili:
1 – Kuramba sahani.
2 – Kuramba vidole.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hauamrishi Ummah wake jambo isipokuwa jambo hilo lina kheri na baraka. Baadhi ya madaktari wamesema kuwa kuramba vidole kwa mabaki ya chakula yaliyobaki kuna faida: kuwepesisha utumbo. Katika vidole hivi kuna zana – kwa idhini ya Allaah – ambazo zinaulainisha utumbo. Tunasema hivi kwa minajali ya kujua ile hekima ya Shari´ah kutokana na yale inayoamrisha. Vinginevyo asli ni sisi kuyapitisha kwa kujisalimisha na yale aliyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Watu wengi hawajui Sunnah hii. Utaona anamaliza kula na sahani alilokulia lote kumebaki mabaki ya chakula. Vilevile utamuona anaenda kuosha mikono bila ya kuramba vidole vyake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mtu asiipanguse mikono yake kwa taulo mpaka airambe na kuisafishe kutokana na chakula kisha baada ya hapo ndio aipanguse kwa taulo halafu baada ya hapo sasa ndio aioshe [kwa maji] ikiwa atataka.
Vilevile miongoni mwa adabu za kula ni pamoja na wakati mtu ataponyokwa na chakula kwenye ardhi, asikiache. Shaytwaan humwendea mwanaadamu katika mambo yake yote; kula, kunywa, jimaa na mengineyo. Anakuwepo katika kila jambo. Usipomtaja Allaah kabla ya kula basi anashirikia na wewe katika kula na mnakula naye pamoja. Kwa ajili hii baraka inaondoshwa katika chakula usipomtaja Allaah.
Unapomtaja Allaah kabla ya kula kisha ukaponyokwa na chakula, shaytwaan anakichukua. Lakini hata hivyo hakichukui na sisi tunaona kwa sababu ni jambo lililofichikana tusilolishuhudia. Lakini hata hivyo tumelijua kupitia katika maelezo ya mkweli anayetakiwa kusadikishwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anakichukua na kukila hata kama kitabaki mbele yetu kihisia, hata hivyo anakila kwa kutoonekana. Haya ni miongoni mwa mambo yaliyofichikana ambayo ni wajibu kwetu kuyasadikisha.
[1]Muslim (2033).
[2]Muslim (2033)
[3]Muslim (2033).
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/298-299)
- Imechapishwa: 18/12/2024

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/298-299)
Imechapishwa: 18/12/2024
https://firqatunnajia.com/hadiyth-hakika-nyinyi-hamjui-baraka-iko-wapi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)