Swali: Baadhi ya wajinga, kama ´Aliy al-Jifriy, amesema ya kwamba kumuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye kaburi lake ni jambo lililowekwa katika Shari´ah na kwamba inafaa kumuomba uokozi baada ya kufa kwake na kwamba yule asiyemuomba uokozi Mtume baada ya kufa kwake anazembea kwa Mtume na kumchukia. Ni upi uhakika wa maneno haya na mtu huyu?

Jibu: Nyinyi, wasio wasomi, wanajua kuwa maneno haya ni batili na kuwa yanaenda kinyume na Qur-aan tukufu yenye kuonesha kuwa Allaah ameharamisha kuwaomba du´aa maiti na kumuomba asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Basi mwombeni Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.” (40:14)

فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.” (72:18)

Haombwi Mtume wala mtu mwengine. Maiti hawaombwi kitu baada ya kufa kwao.

Huyu ni mjinga na maneno yake hayakubaliki. Ni mtu asiyetambulika. Sio katika wanachuoni wa waislamu. Bali ni katika wapotevu. Isitoshe hana hata elimu. Hawezi kuwekwa katika katika kitengo cha wanachuoni wapotevu mpaka isemwe kuwa ni mwanachuoni mpotevu. Hana elimu yoyote. Haya yamedhihiri katika maneno yake na kuonekana kuwa hana elimu yoyote. Ni kitu chenye kuonekana katika maneno yake na kupitia mihadhara yake. Ni mjinga asiyejijua. Mtu asidanganyike naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (17) http://alfawzan.af.org.sa/node/2110
  • Imechapishwa: 09/07/2020