Funika chakula kabla hujaenda kulala na usikile utaposahau kukifunika

Swali: Je, imeamrishwa kufunika matunda na mambogamboga kabla ya kulala?

Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kufunika vyombo vya jikoni na kutaja jina la Allaah wakati wa kufanya hivo. Hivyo ndivo inavotakiwa kufanya sawa ikiwa ni kinywaji au chakula kikavukavu. Isipokuwa tu matunda na mbogamboga zilizo na maganda yake.

Swali: Ni sawa kula chakula hicho ikiwa mtu amesahau kukifunika?

Jibu: Akisahau kufunika chakula hicho basi akipeane kwa wanyama. Asikile. Akikila basi amejifanyia vibaya juu ya nafsi yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Razzaaq bin ´Afiyfiy al-´Afiyfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa wa Rasaa-il-ush-Shaykh ´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy (1/228-229)
  • Imechapishwa: 24/03/2019