Swali: Ni ipi hukumu mke wa kaka kukaa pamoja na familia katika wakati maalum kama wakati wa chakula cha jioni au chakula cha usiku pamoja na kujua ya kwamba mume wake yuko pamoja nasi na kwamba baba, mama na ndugu wengine wote wako pamoja nasi? Lakini hata hivyo anafunika mwili wake wote mbali na uso na vitanga vya mikono ndivyo vinavyokuwa wazi.
Jibu: Naona kuwa familia kukusanyika kwa ajili ya chakula hakuna neno. Lakini wasile kwenye sinia moja ya chakula. Bali wanawake wawe upande mmoja na wanaume wawe upande mwingine hata kama watakuwa sehemu moja. Ama kukaa kwenye sinia moja ya chakula ni jambo tusiloona kuwa lafaa kabisa kabisa. Kwa kuwa mtu hawezi kula pasi na kuacha wazi uso wake[1]. Akiacha wazi uso wake mbele ya kaka wa mume wake, ami yake na watu mfano wao, kunatokea fitina. Usidharau kitu katika shari. Ni watu wangapi ambao wamejitenga mbali kabisa kusitokee fitina kati yao na kati ya wake wa kaka zao, lakini shaytwaan anaweza kuchochea kati yao!
Tazama maneno ya mbora wa viumbe (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) wakati aliposema:
“Tahadharini kuingia sehemu walioko wanawake!”
Sentesi hii ni ya matahadharisho.
“Tahadharini kuingia sehemu walioko wanawake!” Wakasema: “Ee Mtume wa Allah! Vipi kuhusu al-Hamuu?” Akasema: “al-Hamuu ni kifo.”
Maana yake ni kwamba mkimbie kama unavyokikimbia kifo. Kuhusu wale waliosema al-Hamuu, ambayo ni mauti, ni lazima yatokee ni kosa. Kila mmoja anajua kuwa makusudio ya ibara hii ni kushtua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyaweka katika ngazi ya kifo na kwamba ni wajibu kumkimbia kwa sababu al-Hamuu, ambaye ni yule mtu aliye karibu na mke, anapoingia nyumbani kwa nduguye, watu hawawezi kumkemea. Jengine ni kwamba hawezi kuogopa anapofungua mlango na kuingia. Kwa ajili hiyo ni wajibu kwa mtu kutahadhari na ndugu wa mke na mwanamke mbele yao awe katika hadhari na aogope uchochezi wa shaytwaan.
[1] Tazama https://www.youtube.com/watch?v=DS_F3RhNw4Y
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/910
- Imechapishwa: 16/09/2018
Swali: Ni ipi hukumu mke wa kaka kukaa pamoja na familia katika wakati maalum kama wakati wa chakula cha jioni au chakula cha usiku pamoja na kujua ya kwamba mume wake yuko pamoja nasi na kwamba baba, mama na ndugu wengine wote wako pamoja nasi? Lakini hata hivyo anafunika mwili wake wote mbali na uso na vitanga vya mikono ndivyo vinavyokuwa wazi.
Jibu: Naona kuwa familia kukusanyika kwa ajili ya chakula hakuna neno. Lakini wasile kwenye sinia moja ya chakula. Bali wanawake wawe upande mmoja na wanaume wawe upande mwingine hata kama watakuwa sehemu moja. Ama kukaa kwenye sinia moja ya chakula ni jambo tusiloona kuwa lafaa kabisa kabisa. Kwa kuwa mtu hawezi kula pasi na kuacha wazi uso wake[1]. Akiacha wazi uso wake mbele ya kaka wa mume wake, ami yake na watu mfano wao, kunatokea fitina. Usidharau kitu katika shari. Ni watu wangapi ambao wamejitenga mbali kabisa kusitokee fitina kati yao na kati ya wake wa kaka zao, lakini shaytwaan anaweza kuchochea kati yao!
Tazama maneno ya mbora wa viumbe (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) wakati aliposema:
“Tahadharini kuingia sehemu walioko wanawake!”
Sentesi hii ni ya matahadharisho.
“Tahadharini kuingia sehemu walioko wanawake!” Wakasema: “Ee Mtume wa Allah! Vipi kuhusu al-Hamuu?” Akasema: “al-Hamuu ni kifo.”
Maana yake ni kwamba mkimbie kama unavyokikimbia kifo. Kuhusu wale waliosema al-Hamuu, ambayo ni mauti, ni lazima yatokee ni kosa. Kila mmoja anajua kuwa makusudio ya ibara hii ni kushtua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyaweka katika ngazi ya kifo na kwamba ni wajibu kumkimbia kwa sababu al-Hamuu, ambaye ni yule mtu aliye karibu na mke, anapoingia nyumbani kwa nduguye, watu hawawezi kumkemea. Jengine ni kwamba hawezi kuogopa anapofungua mlango na kuingia. Kwa ajili hiyo ni wajibu kwa mtu kutahadhari na ndugu wa mke na mwanamke mbele yao awe katika hadhari na aogope uchochezi wa shaytwaan.
[1] Tazama
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/910
Imechapishwa: 16/09/2018
https://firqatunnajia.com/familia-ya-mume-kuchangia-chakula-na-mke-wa-mume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)