139 – Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Ammaar ametukhabarisha: Mu´aafaa bin ´Abdir-Rahmaan ametukhabarisha, kutoka kwa Sulaymaan bin Bilaal, kutoka kwa Suhayl bin Abiy Swaalih, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Bora ya mtu ni Abu Bakr! Bora ya mtu ni ´Umar! Bora ya mtu ni Abu´Ubaydah bin al-Jarraah! Bora ya mtu ni Thaabit bin Qays! Bora ya mtu ni Mu´aadh bin ´Umar bin al-Jamuuh! Bora ya mtu ni Mu´aadh bin Jabal! Bora ya mtu ni Sahl bin Baydhwaa’!”[1]

140 – Ahmad bin Sa´iyd ametukhabarisha: Ya´quub bin Ibraahiym ametukhabarisha: Baba yangu ametukhabarisha: Yaziyd bin al-Haad amenihadithia: ´Abdullaah bin Khabbaab amemuhadithia: Abu Sa´iyd al-Khudriy amemuhadithia:

“Usiku mmoja Usayd bin Hudhwayr alipokuwa kwenye duka la tende akisoma, farasi wake alianza kukimbia. Akaanza kusoma tena ambapo akakimbia. Akaanza kusoma tena ambapo akakimbia. Usayd akasema: “Niliogopa ingemkanyaga Yahyaa na nikasimama kumwendea. Ghafla nikaona kitu kama wingu juu ya kichwa changu. Ilikuwa na kitu kama mwanga. Iliinuka angani na kutoweka machoni pangu. Asubuhi iliyofuata nilikwenda kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Usiku uliopita nilikuwa kwenye duka langu la tende wakati farasi wangu alipoanza kukimbia.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Nisomee, ee mwana wa Hudhwayr!” Nikasoma. Yahyaa alikuwa karibu nayo, nikachelea kwamba asimkanyage. Kisha nikaona kitu kama wingu juu ya kichwa changu. Ilikuwa na kitu kama mwanga. Iliinuka angani na kutoweka machoni pangu. Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Hao walikuwa ni Malaika. Walikuwa wanakusikiliza. Lau ungeendelea kusoma, basi watu wangewaona asubuhi iliyofuata – wasingejificha kwao.”[2]

[1] at-Tirmidhiy (3795), aliyesema Hadiyth ni nzuri, na al-Haakim (3/233 na 268), ambaye amesema Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti ya Muslim. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3795).

[2] al-Bukhaariy (4730) na Muslim (796).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 16/09/2026