134 – Muhammad bin ´Abdil-A´laa ametukhabarisha: Khaalid ametukhabarisha: Shu´bah ametukhabarisha, kutoka kwa Qataadah: Nimemsikia Anas akisema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Ubayy bin Ka´b:

”Allaah (´Azza wa Jall) ameniamrisha nikusomee Qur-aan.” Akasema: ”Amenitaja kwa jina?” Akasema: ”Amekutaja kwa jina.” Akaanza kulia.”[1]

135 – Muhammad bin Yahyaa bin Ayyuub ametukhabarisha: Sulaymaan bin ´Aamir ametukhabarisha: Nimemsikia ar-Rabiy´ bin Anas akisema:

“Nilimsomea Qur-aan Abul-´Aaliyah na Abul-´Aaliyah akamsomea Qur-aan Ubayy. Ubayy akasema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  aliniambia: “Nimeamrishwa nikusomee Qur-aan.” Akasema: ”Je, nimetajwa huko?” Akasema: “Ndio.” Ubayy akalia.” Akasema: “Sijui alifanya hivo kwa furaha au kwa khofu.”

136 – ´Amr bin ´Aliy ametukhabarisha: Yahyaa ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha: Salamah bin Kuhayl ametukhabarisha, kutoka kwa Dharr, kutoka kwa Sa´iyd bin ´Abdir-Rahmaan bin Abzaa, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliswali Fajr na kuna Aayah akaiacha ambapo akasema: “Je, Ubayy bin Ka’b yuko katika watu?” Akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, umeisahau Aayah kadhaa na kadhaa au imefutwa? Akasema: “Nimeisahau.”[2]

137 – Muhammad bin Aadam bin Sulaymaan ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Mu´aawiyah, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Shaqiyq, kutoka kwa Masruuq, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jifunzeni Qur-aan kwa watu wanne: ”Ibn Mas´uud, Ubayy bin Ka’b, Mu´aadh bin Jabal, Saalim, mtumwa wa Abu Hudhayfah.”[3]

138 – Ahmad bin Sulaymaan ametukhabarisha: ´Affaan bin Muslim ametukhabarisha: Wuhayb ametukhabarisha: Khaalid al-Hadhdhaa’ ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Qilaabah, kutoka kwa Anas, aliyesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu mwenye rehema zaidi wao katika ummah wangu kwa ummah wangu ni Abu Bakr. Mshupavu zaidi wao katika amri ya Allaah ni ´Umar. Mwenye aibu zaidi wao ni ´Uthmaan. Mwenye kukisoma zaidi wao Kitabu cha Allaah ni Ubayy bin Ka’b. Mjuzi zaidi wao katika fani ya mirathi ni Zayd bin Thaabit. Mjuzi zaidi wao juu ya halali na haramu ni Mu’aadh bin Jabal. Zindukeni! Hakika kila ummah una mtu mwaminifu. Hakika mwaminifu wa ummah huu ni Abu ´Ubaydah.”[4]

[1] al-Bukhaariy (4960) na Muslim (799).

[2] Ahmad (3/408). al-Haythamiy amesema:

“Ameipokea Ahmad na at-Twabaraaniy kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abzaa. Wapokezi wake ni wapokezi wa Swahiyh.” (Majma´-uz-Zawaa-id (2/69))

[3] al-Bukhaariy (3758) na Muslim (2464).

[4] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (868).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 95-97
  • Imechapishwa: 16/09/2026