Swali: Ni yepi maoni yako kwa mwenye kusema kwamba wanawake hawatomuona Allaah siku ya Qiyaamah?

Jibu: Hili ni kosa. Watu wote, waumini wa kiume na wa kike, watamuona Allaah. Wote watamuona Mola wao (Subhaanah) siku ya Qiyaamah na Peponi. Hii ndio neema kubwa kabisa kwa watu wa Peponi. Amesema (´Azza wa Jall):

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya mazuri watapata Pepo na zaidi.” (10:26)

Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba ziada ni kuona uso wa Allaah. Ziada ni Pepo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh pindi Maswahabah walipomuuliza:

”Je, tutamuona Mola wetu?” Akasema: ”Je, mnadhurika mnapotazama jua kweupee kusipokuwa mawingu?” Wakajibu: ”Hapana.” Akasema: ”Je, mnadhurika mnapotazama mwezi usiku wa mwezi mkubwa kweupee kusipokuwa mawingu?” Wakajibu: ”Hapana.” Ndipo akasema: ”Basi vivyo hivyo nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyoona mwezi na jua.”

Hili ni kwa wanamme na wanawake wote. Isitoshe ni miongoni mwa neema. Wao ni wenye kushiriki katika neema. Wanamme na wanawake ni wenye kushirikiana katika neema. Hii pia ni neema. Bali ndio neema ilio juu zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4400/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B2%D8%B9%D9%85-%D8%A7%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%B3%D8%A7%D8%A1-%D9%84%D8%A7-%D9%8A%D8%B1%D9%8A%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%82%D9%8A%D8%A7%D9%85%D8%A9
  • Imechapishwa: 11/10/2020