Elimu ya kidunia ni sawa na elimu ya dini?

Swali: Mwanafunzi anayesoma elimu za kidunia; kama fizikia, udaktari na mambo ya mazoezi ana daraja moja kama mwanafunzi anayesoma Dini; kama Fiqh na mengineyo?

Jibu: Hapana. Hayo ni mambo yenye kuruhusiwa [mubaah] tu tofauti na elimu na Kishari´ah ambayo ni ´Ibaadah. Hii sio sawa na hii. Kusoma elimu za kidunia ni jambo ambalo limeruhusiwa ambalo mtu hapati thawabu kwa kulifanya wala hapati adhabu. Kwa kuwa mambo yenye kuruhusiwa hayako sawa, yanatofautiana. Hilo – elimu ya kidunia – linaingia ndani ya mambo ambayo mtu hapati thawabu wala adhabu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-08.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014