Lau leo mtu atamkata mwenye kufanya mambo kama haya – yaani msimamo wa Imaam Ahmad kwa waliotikia fitina wakati wake – msusaji ataambiwa kuwa ni mwenye msimamo mkali, mpetukaji mipaka, mkosoaji na mwenye kujeruhi. Pamoja na kuwa wengi wanaojinasibisha na Sunnah hii leo wamekosolewa. Hata kama watajinasibisha na Sunnah. Bali hatuoni ukali wao isipokuwa tu kwa Ahl-us-Sunnah na wakati huohuo wanawapa udhuru Ahl-ul-Ahwaa´, kuwatetea na kuyatakasa makosa yao. Sivyo tu bali wakati mwingine utawasikia wakisema kuwa ni Salafiyyuun na mwingine utamsikia anasema kuwa hawawezi wakawatoa katika Salafiyyah. Wamewafungulia vifua vyao watu hawa na wakati huohuo Salafiyyuun hawakusalimika na ndimi zao. Aina hii ya watu ndio khatari zaidi kwa Salafiyyuun kuliko Ahl-ul-Ahwaa´ wal-Bid´ah. Ndugu zangu, tahadharini nao kabisa. Utayemsikia akizungumza maneno kama haya na hawafungulii kifua chake Ahl-us-Sunnah na kuwapa udhuru na badala yake anafanya hivo kwa wale watu waliopondwa basi ni mwongo. Haijalishi kitu hata kama atakuwa na kilemba chenye kufika mbinguni.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=5503
  • Imechapishwa: 27/08/2020