Du´aa za makafiri kuwaombea waislamu

Muslim na Ahmad wamepokea kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ndio, nimewasikia ambapo nikawajibu. Du´aa zetu dhidi yao zinajibiwa na du´aa zao dhidi yetu hazijibiwi.”

Baada ya Hadiyth hii Ibn Raahuuyah amepokea kwamba Hassaan bin ´Atwiyyah amesema:

“Hakuna neno kusema “Aamiyn” juu ya du´aa ya mtawa pindi anapokuombea du´aa. Du´aa zao kwetu zinaitikiwa na hawaitikiwi wakiomba kwa nafsi zao wenyewe.”

Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/1/493)
  • Imechapishwa: 22/08/2020