Du´aa ya kuwaombea wenyeji wako baada ya chakula

Swali: Ukila kwa watu unatakiwa uwaambie:

اللهم بارك لهم فيما رزقتهم

”Ee Allaah! Wabariki katika kile ulichowaruzuku.”?

Jibu: Akila kwa watu awaombee du´aa kwa kusema:

اللهم بارك لهم فيما رزقتهم واغفر لهم وارحمهم، أكل طعامكم الأبرار، وأفطر عندكم الصائمون، وصلت عليكم الملائكة

”Ee Allaah! Wabariki katika kile ulichowaruzuku na uwasamehe na uwarehemu. Wale chakula chenu watu wema, wafuturu kwenu waliofunga na wawaombee du´aa Malaika.”

Haya yanahusiana atayowaambia watu. Kuhusu yanayohusiana na yeye, amuhimidi Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23999/هل-يستحب-لمن-طعم-عند-اناس-الدعاء-لهم
  • Imechapishwa: 15/08/2024