Du´aa ya kufungulia swalah kila baada ya Rak´ah mbili

Swali: Je, inafaa kutosheka na du´aa moja ya kufungulia swalah katika swalah ya Tarawiyh? Je, ipo du´aa maalum ya kufungulia swalah kwa ajili ya swalah ya usiku inayotofautiana na swalah ya faradhi na swalah ya Tarawiyh?

Jibu: Inapendeza kusoma du´aa ya kufungulia swalah kila baada ya Tasliym ya swalah ya Tarawiyh. Kwa sababu kila Tasliym ni swalah yenye kujitegemea tofauti na iliokuwa kabla yake. Namna ya du´aa ya kufungulia hapana tofauti kati ya swalah ya faradhi na swalah ya sunnah. Du´aa ya kufungulia inakuwa kwa moja wapo ya zile du´aa za kufungulia swalah zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Iliotangaa zaidi ni:

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ وتَبَارَكَ اسْمُكَ وَتَعَالى جَدُّكَ وَلا إِله غَيْرُكَ

“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah, kutokamana na kasoro zote na himdi zote ni Zako. Limetukuka jina Lako, ufalme Wako ni mkubwa na hapana mungu wa haki mwengine asiyekuwa Wewe.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (06/78)
  • Imechapishwa: 22/04/2022