Du´aa ya adhaana baada ya kukimiwa swalah

Swali: Du´aa inayotambulika inayosomwa baada ya adhaana[1] inasomwa pia baada ya Iqaamah?

Jibu: Ndio, kwa sababu Iqaamah pia ni adhaana timilifu. Iqaamah ni utambulisho wa kuwadia wakati wa kuswali. Adhaana ni utambulisho wa kuwadia kuingia wakati wa swalah. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ipo swalah baina ya kila adhaana mbili.”

 Iqaamah pia huitwa adhaana.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/15-adhkaar-za-adhaana/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 06/11/2020