Swali: Je, usuniwaji wa du´aa ni wenye kuendelea wakati waislamu wanapofikwa na janga?

Jibu: Ndio. Hata hivyo watu wabainishiwe kuwa uamuzi ni wa Allaah na kwamba wao kinachowawajibikia ni kuomba du´aa. Uamuzi uko mikononi mwa Allaah na kwamba hawawezi kupata ushindi kwa mikono yao. Uamuzi uko mikononi mwa Allaah. Waja wanachotakiwa ni wao kuomba du´aa, kupambana jihaad, kujiandaa na kuwafikishwa kuko mikoni mwa Allaah. Anamnusuru amtakaye, wakati mwingine anachelewesha ushindi na wakati mwingine anauleta mapema. Yeye ndiye Mwingi wa hekima, Mjuzi wa kila jambo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24312/ما-حكم-الدعاء-في-النوازل
  • Imechapishwa: 28/09/2024